Apply Now

Login Form

Visitors Counter

205762
Today
Yesterday
This Week
Last Week
This Month
Last Month
All days
90
238
644
203851
4120
7317
205762

Your IP: 100.26.196.222
2024-02-21 14:52

Leo Tarehe 20.07.2021 Chuo cha Afya HERMARGS kimepata bahati ya kutembelewa na ugeni mkubwa kwa ngazi ya Wilaya yetu ya Mvomero ikiongozwa na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ndugu Halima Okash. Pia Mh. Mkuu wa Wilaya aliongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ndugu Hassani Njaama na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya. Aidha katika ziara hiyo pia kulikuwa na wataalamu mbalimbali kutoka ofisi ya Mkurugenzi na wenyeji Kata ya Mlali ambapo Chuo kipo.

Lengo kubwa la ujio wake Chuoni kwetu pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kujitambulisha kwani Mkuu wa Wilaya leo ametimiza mwezi mmoja tangu ateuliwe na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo Wilayani Mvomero. Kwetu sisi ni bahati kubwa kwani katika taasisi ambazo Mh. Mkuu wa Wilaya amepanga kuzitembelea na kujitambulisha nasi HERMARGS ni mojawapo.

Katika hotuba yake ya utambulisho, Mh. Okash ameeleza kufurahishwa kwake namna chuo kilivyojengwa pamoja na kuwashukuru wamiliki wa Chuo wakiwakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Prof. Robinson Mdegela. Pia Mh. Mkuu wa Wilaya aliona namna wanafunzi wanavyofundishwa kwa kwa vitendo kwa kutumia maabara ya kisasa ya mafunzo ya kutengeneza dawa; na pia maabara nzuri kwa ajili ya mafunzo ya TEHAMA. Aidha wanafunzi hao walionyesha kwa vitendo namna ya kutengeneza vitakasa mikono yaani “Sanitizer” kwa ajili ya kupambana na ugonjwa hatari wa UVIKO 19. Mh. Mkuu wa Wilaya pia aliwapongeza wafanyakazi wa Chuo kwa kujitoa na kufundisha vijana ili kupata ujuzi maarifa yaliyo sahihi ya kuwezesha kuajiriwa au kujiajiri na kujitegemea mara tu baada ya kumaliza masomo yao. Mkuu wa Wilaya alikishukuru chuo na uongozi mzima kwa namna wanavyoshirikiana vizuri na jamii inayokizunguka kwa kutoa michango mbalimbali katika Shule za msingi Kinyenze na Kipera na Sekondari ya Kipera, Kijiji cha Kinyenze na Kipera na Kata ya Mlali kwa ujumla. Mh. Mkuu wa Wilaya alihimiza pia wananchi na wanajumuiya wote wa HERMARGS kuchukua tahadhari ya UVIKO-19 (virusi vya CORONA – 19) ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni za Afya juu ya UVIKO-19.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya HERMARGS MDEGELA ACADEMY LTD Profesa Robinson Mdegela kwa niaba ya wenzake alimshukuru Mkuu wa Wilaya, Kamati ya Ulinzi na Usalama na msafara wake wote uliokuwepo kwa kututembelea na kukazia kuwa “Elimu inayotolewa inalenga kumjengea uwezo mwanafunzi aweze kupata ujuzi na maarifa ya kujitegemea kwa kujiajiri mwenyewe” dhana ambayo aliiasisi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Pia alimkaribisha Mh. Mkuu wa Wilaya na msafara wake kufika HERMARGS kadiri wanapopata nafasi.

Imeandaliwa na:

CLEOPA MDEGELA

AFISA TAWALA WA CHUO

Whatsapp Apply

Tuma form iliyojazwa kwa whatsapp baada ya kuiscan pamoja na viambatanisho kwenye No: +255743494346 au 787047650